NABI AWAPA TANO KAGERA SUGAR

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amewapa pongezi Kagera Sugar kwa kuonyesha ushindani kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Dakika 90 zimekamilika, ubao umesoa Kagera Sugar 0-1 Yanga bao ambalo lilifungwa mapema kipindi cha kwanza.

Ni Clemet alipachika bao hilo dakika ya 18 lililomshinda kipa wa Kagera Sugar Said Kipao.

Kipindi cha pili kipa wa Yanga, Diarra Djigui aliokoa mchomo wa penalti dakika ya 70 na kulifanya lango kuwa salama.

Yanga inafikisha pointi 23 ikiwa ni namba moja kwenye msimamo na haijapoteza mchezo msimu wa 2022/23