JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa kazi ambayo anaifanya Victor Ackpan raia wa Nigeria kwenye kikosi hicho siyo ya kubezwa itaonyesha matokeo hivi karibuni.
Nyota huyo hakuwa chaguo la kwanza la Mgunda kwenye mechi za hivi karibuni na alianzia benchi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 5-0 Mtibwa Sugar.
Mgunda amesema kuwa anatambua uwezo wa wachezaji waliopo ndani ya Simba pamoja na kile ambacho wanakionyesha mazoezini.
“Nilikuwa na kijana wangu Akpan ndani ya Coastal Union na alikuwa ni chaguo la kwanza bahati nilipokuja Simba hajapata muda mrefu wa kucheza kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha lakini sasa amepona.
“Ukweli ni kwamba uwezo wake unaonekana ni mtu anayejua kazi yake na unajua kwamba mchezaji yoyote aliyesajiliwa ndani ya Simba uwezo wake ni mkubwa na ni lazima aweze kucheza hivyo atacheza na ataonekana uwanjani kwa dakika zozote atakazopewa,” amesema Mgunda.