CLATOUS Chama nyota wa Simba atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars unaotarajiwa kuchezwa kesho Novemba 9,2022 Uwanja wa Liti.
Sababu ya nyota huyo kukosekana kwenye mchezo huo ni maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania ambayo yametolewa kutokana na kikao cha Novemba 4,2022.
Kamati imemfungia nyota huyo kwenye jumla ya michezo mitatu na atatozwa faini ya laki tano.
Nyota huyo kwenye mchezo uliochezwa Oktoba 23,2022 alifanya kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo huo uliokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.