MAN UNITED YAPATA TABU MBELE YA VILLA

 ASTON Villa ikiwa Uwanja wa Villa Park imewashushia balaa zito Manchester United kwa kufunga mabao yote manne wakati wakishinda 3-1.

Ni Leon Bailey alipachika bao la ufunguzi dakika ya 7 kisha Lucas Diagne alipachika bao la pili dakika ya 11.

Pia mabao mawili yalifungwa kupitia kwa Jacob Ramsey wa Villa ambaye alijifunga dakika ya 45 na bao la tatu kwa Villa lilifungwa na yeye mwenyewe dakika ya 49 na kumfanya afute makosa yake.

Man United inafikisha pointi 23 ikiwa nafasi ya tano na Villa inafikisha pointi 15 ikiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo.