>

MZAWA SIMBA APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

 MZAWA Mzamiru Yassin amechaguliwa kuwa mchezaji bora kwa mwezi Oktoba.

Ni kupitia tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Oktoba.

Nyota huyo amewashinda wenzake ambao waliingia nao fainali ya kuwania tuzo hiyo ikiwa ni Joash Onyango na Augustine Okrah.

Kiungo huyo ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Juma Mgunda ambaye ameweka wazi kuwa ni moja ya wachezaji wanaotimiza majukumu kwa umakini.

Mzamiru alikosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC na ulikuwa ni wa kwanza kupoteza Simba kwenye ligi kwa kunyooshwa bao 1-0.

Alirejea kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar wakati Simba ikishinda mabao 5-0 alitupia bao moja na alitoa pasi moja ya bao.

Kwa sasa Simba ipo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti.