>

AZAM FC YASEPA NA POINTI TATU ZA SIMBA

AZAM FC wameupiga mpira mwingi kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Simba na kufanikiwa kusepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Pongezi kwa Prince Dube ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 35 kwenye mchezo huo ambapo Simba walikuwa hawapo kwenye ubora wao.

Kwenye kila idara Simba leo walikuwa wamezidiwa kuanzia viungo wa kati, pembeni pamoja na ile ya ulinzi ambapo jitihada za Joash Onyango, Aishi Manula zingekuwa hafifu wangepoteza kwa kufungwa mabao zaidi ya mawili.

Ni Habib Kyombo atajilaumu mwenyewe kwa kukosa nafasi ya wazi dakika ya tatu ya mchezo kwa pasi ya Augustino Okra.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu wa 2022/23 na ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Juma Mgunda kuonja joto ya jiwe ya kupoteza pointi tatu.