ULIMWENGU wa mpira unasubiri kuona mpira wa kiungwana mbele ya watani wa jadi Simba na Yanga ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 23,2022 Uwanja wa Mkapa.
Mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2022/23 na kila timu imetoka kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hapa tunaamini kwamba kila mchezaji ana kitu cha kufanya.
Wachezaji kwenye mechi za hivi karibuni walikuwa wakionyesha ubabe mwingi badala ya kucheza kwa umakini kwa kufuata sheria za mpira.
Pia matukio yale ya kufanyiana vitendo ambavyo sio vya kiungwana uwanjani vimekuwa vikionekana kwenye mechi hizi kubwa kwa wakati huu inatosha.
Kushiriki mashindano ya kimataifa ni mwanzo wa kufanya kazi kwa umakini ili kuongeza nguvu kwenye anga za kimataifa kwa kuwa kila dunia inausubiri mchezo huo.
Tunaamini wakati huu wa maandalizi wachezaji watapitia kanuni vizuri na kucheza kwa umakini kupata matokeo kwenye mchezo huo.
Mshindi wa kweli ni yule ambaye atatumia makosa ya mpinzani na yule atakayepoteza ama kushinda akubali matokeo kwani huwezi kubadili yakitokea.
Kila la kheri kuelekea kwenye maandalizi ya mchezo huo wa ligi ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki.