JUMA MGUNDA HESABU ZAKE KWA WANANCHI

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa kwa sasa akili zake ni kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga.

Mgunda anafanya kazi kwa ushirikiano na Seleman Matola wote wakiwa ni wazawa wamefanikiwa kukiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Oktoba 23,2022 Uwanja wa Mkapa mchezo wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa ambapo kila timu inahitaji pointi tatu muhimu.

Mgunda ameweka wazi kuwa walikuwa wanapiga hesabu kwenye mechi zao za kimataifa jambo lililowafanya wafanye vizuri baada ya kazi kuisha sasa wanarejea kwenye ligi.

“Kwenye kila mchezo ambao unatukabili ni muhimu kufanya maandalizi mazuri na ninajua kwamba wapinzani wangu, (Yanga) wapo imara hivyo nasi tunajipanga kupata matokeo.

“Kikubwa ni utayari na wachezaji wanajua kwamba kuna haki na wajibu, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza,”.

Mgunda amebainisha kuwa anawatambua wapinzani wake Yanga kwa kuwa amekutana nao mara nyingi kabla hajawa ndani ya Simba.

Timu zote ndani ya ligi baada ya kucheza mechi tano zimekusanya pointi13 na hakuna timu ambayo imepoteza mchezo wake msimu wa 2022/23.