UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kwa sasa akili zote zinaelekezwa kwenye mechi za Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushindwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi iliondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa ilikubali sare ya bao 1-1 na ule wa pili ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Rais wa Yanga, Hers Said amesema kuwa hakuna wa kumlaumu kwa kushindwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo wanajipanga Kombe la Shirikisho.
“Tumeshindwa kupata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Al Hilal hatuna wa kumlaumu kwa sasa hivyo kikubwa ni kujipanga kwa ajili Kombe la Shirikisho ambalo nalo ni mechi za kimataifa.
“Sisi kauli mbiu yetu kubwa ni daima mbele nyuma mwiko hivyo tunaendelea mbele na yale makosa ambayo yametokea nina amini benchi la ufundi litayafanyia kazi ili kuwa imara kwa wakati ujao,” .
Miongoni mwa nyota ambao walianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Al Hilal ni pamoja na Bernard Morrison, Fiston Mayele na Aziz KI.