DAKIKA 540 ambazo ni mechi sita, Ihefu ilicheza bila kuambulia ushindi ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.
Jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya Melis Medo aliyechukua mikoba ya Masoud Djuma.
Uwanja wao wa nyumbani wa Highland Estate ulichezwa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Ni mabao ya Jaffary Kibaya dakika ya 22 na Obrey Chirwa dakika ya 33 yalitosha kuipa ushindi Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.