SIMBA imetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya de Agosto.
Mchezo wa ugenini Simba ilishinda kwa mabao 3-1 na leo Oktoba 16,2022 imeibuka na ushindi wa bao 1-0.
Ushindi huo wakiwa nyumbani unawapa tiketi ya kufuzu hatua ya makundi chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda.
Bao la ushindi ni mali ya Moses Phiri ambaye alifunga bao hilo dakika ya 33 Uwanja wa Mkapa.
Miongoni mwa wachezaji ambao walianza kikosi cha kwanza ni pamoja na kiungo Pape Sakho, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.