MATOKEO ya mechi za Ligi Kuu Bara leo Oktoba 15,2022 yapo namna hii:-
KMC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Ni mabao ya Irahim Ame dakika ya 39 na Emmanuel Mvuyekule dakika ya 58.
Kwa upande wa bao la Mtibwa Sugar mtupiaji ni Charlse Ilanfya dakika ya 12.
Mchezo mwingine Kagera Sugar imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Hamis Kiza alifunga bao moja dakika ya 9 na bao la pili ni Anuary Jabir alifunga dakika ya 69 huku lile la Ruvu Shooting likifungwa na Rashid Juma dakika ya 27.