MSHAMBULIAJI Fiston Mayele kwenye anga za kimataifa ni mabao 7 katupia katika mechi tatu za ushindani ambazo Yanga imecheza.
Mayele amefunga mabao hayo kwenye mchezo dhidi ya Zalan FC ya Sudan katika mechi mbili ni mabao sita aliwafunga, mchezo wa kwanza alifunga mabao matatu na ule wa pili alifunga mabao matatu.
Yanga ilitinga raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 9-0 na mabao mengine matatu yalifungwa na Aziz KI, Feisal Salum na Farid Mussa.
Bao la saba Mayele alifunga dhidi ya Al Hilal kwenye mchezo wa raundi ya Pili, kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Mkapa.
Kibarua kilicho mbele ya Yanga inayonolewa na Nasreddine Nabi ni kupata matokeo ugenini ili kufungua ukurasa wa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 16,2022 ambapo kwa sasa kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo.
Mayele amesema kuwa wanatambua kazi ni kubwa kimataifa na malengo yao ni kupata matokeo.
“Kazi ni kubwa na ushindani pia ni mkubwa tunakwenda ugenini kutafuta ushindi mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.