STAA wa Simba Moses Phiri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika mechi tatu kacheka na nyavu mara nne wakati timu hiyo ikipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Alifunga kwenye mchezo dhidi ya Big Bullets kwenye hatua ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wa kwanza alitupia bao moja ugenini na mchezo wa pili Uwanja wa Mkapa alitupia mabao mawili.
Simba inayonolewa na mzawa Juma Mgunda ilitinga hatua ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-0 Big Bullets ilitupa kete ya kwanza ugenini dhidi ya de Agosto ya Angola na kushinda mabao 3-1.
Katika ushindi huo, Phiri alifunga bao moja na kufikisha mabao manne kimataifa akiwa ni namba moja kwa watupiaji wa Simba.
Ikiwa imefunga mabao 7 kimataifa mabao matatu ni mali ya John Bocco ambaye ni nahodha, Israel Mwenda beki wa kupanda na kushuka na kiungo Clatous Chama.
Phiri amesema kuwa hayo yote yanatokana na ushirikiano ambao anaupata kutoka kwa wachezaji wenzake.
“Tunashirikiana kwenye majukumu yetu na ninapenda kuona tunazidi kupata matokeo hilo linawezekana kwa kuwa pamoja,”.
Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya de Agosto, Jumapili Oktoba 16, Uwanja wa Mkapa.