AZAM FC MATUMAINI KIBAO KUWAKABILI WAARABU

BAADA ya kupoteza ugenini kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Akhadar ya Libya, Azam FC hesabu zao ni kupata matokeo nyumbani.Wakiwa ugenini walikubali kipigo cha mabao 3-0 jambo ambalo linawafanya wawe na kibarua cha kusaka ushindi wa zaidi ya mabao matatu bila kufungwa wakiwa Azam Complex.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Denis Lavagne ameweka wazi kuwa makosa ambayo wamefanya watafanyia kazi kupata matokeo.

“Kuna makosa tulifanya kwenye mchezo wetu wa kwanza na tayari tumeshayafanyia kazi kikubwa ni kwamba tupo tayari kwa mchezo huo,”.

Tayari kikosi kimeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo kuwakabili waarabu wa Libya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 kwenye hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika.