SIMBA USHAMBULIAJI IMEKIMBIZA, PHIRI NAMBA MOJA

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kimekuwa na moto kwenye safu ya ushambuliaji huku ukuta wao ukiwa haujaruhusu mabao mengi kwenye mechi za ushindani.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 8 za mashindano, ligi mechi tano na Ligi ya Mabingwa Afrika mechi tatu imetupia jumla ya mabao 18 huku safu ya ulinzi ikiwa imeokota nyavuni mabao matatu.

Kwenye mabao 11 ambayo Simba imefunga kwenye ligi na mabao 7 ambayo imefunga kimataifa, Israel Mwenda ni beki wa kwanza kufunga bao msimu huu ikiwa ni rekodi mpya na alifunga ugenini dhidi ya de Agosto ya Angola.

Mabao 11 kwenye ligi ambayo yamefungwa ni Moses Phiri anaongoza akiwa nayo manne, Habib Kyombo anayo mabao mawili, Agustino Okra, Clatous Chama, Jonas Mkude, Dejan ambaye amesepa Simba hawa wote walifunga bao mojamoja huku Abdalah Shaibu wa Dodoma Jiji akijifunga bao moja.

Kwa upande wa mabao ya kimataifa ni Phiri kafunga mabao manne, Bocco bao moja,Chama bao moja na Mwenda ni beki wa pembeni amekabidhiwa mikoba ya Shomari Kapombe ambaye kwa sasa bado hajawa fiti.

Phiri anaongoza chati ya ufungaji akiwa na jumla ya mabao nane kwenye mashindano yote huku Kyombo na Chama wakifuatia wakiwa wametupia mabao mawilimawili.

Mgunda amesema kuwa kinachohitajika uwanjani ni kutumia nafasi ambazo zinatangenezwa ili kupata ushindi.

“Kwanza ni kutegeneza nafasi na kuzitumia, suala la nani anafunga hilo ni la kila mmoja, kikubwa tunaona kila mchezaji anatimiza majukumu yake ni hicho kinahitajika kwenye kila mechi,” .