MECHI ZA SIMBA, YANGA, AZAM KUPANGIWA TAREHE UPYA

MICHEZO mitatu ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 itapangiwa tarehe mpya tofauti na ile ya awali ambayo imepangwa.

Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imeeleza kuwa imeamua kufanya hivyo kuzipa muda timu shiriki kimataifa kufanya maandalizi.

Mechi hizo ilikuwa ni pamoja na ule mchezo wa Singida Big Stars dhidi ya Simba awali ulitarajiwa kuchezwa Oktoba 12, Uwanja wa Liti.

Pia mchezo wa Azam FC v Dodoma ambao ulitarajiwa kuchezwa Oktoba 12, Uwanja wa Azam Complex.

Ule wa tatu ni Namungo v Yanga ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Oktoba 13.

Pia Bodi ya Ligi ya Ligi imewatakia maandalizi mema wawakilishi wa Tanzania kimataifa.