BREAKING: MZUNGU WA SIMBA MKATABA WAKE WAVUNJIKA

DEJAN Georgijevic maarufu kama Mzungu wa Simba amebainisha kuwa mkataba wake na mabosi hao umevunjika kutokana na makubaliano ya kimkataba.

Nyota huyo kwa sasa yupo na kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Zanzibar kwa ajili ya mechi za kirafiki mchezo wa kwanza walishinda bao 1-0 dhidi ya Malindi na leo wanatarajia kucheza dhidi ya Kipanga FC.

Kwenye mchezo dhidi ya Malindi FC alipofanyiwa mabadiliko yeye pamoja na Agustino Okra wakati wakitoka walionekana kuzozana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni tofauti za kawaida zilizotokea kwenye mchezo huo kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mshambuliaji huyo amebainisha kwamba:”Ninathibitiha kwama mkataba wangu wa ajira umevunjwa kutokana na sababu zilizokuwa kwenye makubaliano yetu na timu.

“Asante mashabiki kwa sapoti ambayo mmenipa pamoja na upendo mlionipa,”.

Mtu wa karibu ndani ya Simba ameweka wazi kuwa taarifa hizo zipo ila zitathibitishwa hivi punde.

“Hilo lipo lakini kuna mipango inawekwa sawa ikiwa litakamilika basi mashabiki watajua kuhusu hilo suala,”