MOHAMED Hussein,nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuendelea kuwa pamoja nao kwenye mechi zote wanazocheza ili kuwapa nguvu ya kupambana.
Simba inapambana kusaka taji la ligi ambalo lipo mikononi mwa Yanga ililotwaa kwa msimu wa 2021/22 bila kupoteza kwenye mechi 30 na ilikusanya pointi 74.
Imerejea Dar kutoka Mbeya ilipokuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons na ilishinda bao 1-0 mtupiaji akiwa ni Jonas Mkude.
Mohamed amesema kuwa kwenye kila mechi ambazo wamekuwa wakicheza na kupewa sapoti na mashabiki kuna jambo huwa linaongezeka na kuwafanya wapambane bila kuchoka.
“Mashabiki ni watu muhimu kweli kwenye mechi ambazo tunacheza, tunaona kwamba walikuwa nasi msimu uliopita licha ya kushindwa kutwaa ubingwa na sasa wanaendelea hilo ni jambo kubwa.
“Wakati huu wazidi kuwa nasi kila hatua tuna amini kwamba tutafanya vizuri, tunajitajidi kutafuta matokeo kwa kushirikiana na wahezaji pamoja na benchi la ufundi kwani tunajua kwamba ushindani ni mkubwa,” amesema Mohamed.
Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Big Bullets ambao ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili, Septemba 18.