NABI ANAAMINI KAZI HAIJAISHA KIMATAIFA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema bado kazi ipo kwenye mchezo wao ujao wa kimataifa dhidi ya Zalan FC.

Jana, Septemba 10, ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ulisoma Zalan 0-4 Yanga huku wafungaji wakiwa ni Fiston Mayele aliyetupia mabao matatu na mzawa Feisal Salum aliyefunga bao moja.

Ushindi huo ulipatikana kipindi cha pili baada ya dakika 45 za mwanzo kila timu kukwama kumtungua mpinzani wake.

Nabi amesema:”Walishindwa kupata mabao ya mapema lakini tumetengeneza nafasi nyingi hiyo ilikuwa imetufanya tushindwe kuongeza hali ya kujiamini lakini kipindi cha pili tumeweza kupiga hatua kubwa.

“Mabadiliko yote ilikuwa ni kipindi cha pili unaona tulipopata bao la kuongoza iliongeza hali ya kujiamini hivyo bado tunazidi kuwa karibu na kutoka kwenye hatua hii kuelekea hatua inayofuata,” amesema.

Wikiendi ijayo timu hizo zinatarajia kurejeana Uwanja wa Mkapa ambapo ni Yanga atakuwa mwenyeji kwenye mchezo ujao.

Mshindi wa jumla atakwenda kukutana na mshindi kati ya Saint George ya Ethiopia ama Al Hilal ya Sudan kwenye hatua ya kwanza kimataifa.