>

USAJILI WA KISINDA MAMBO BADO

IMEELEZWA kuwa nyota mpya wa kikosi cha Yanga, Tuisila Kisinda hatakuwa sehemu ya kikosi cha msimu mpya wa 2022/23 kutokana na usajili wake kushindwa kukamilika.

Usajili huo umekwama kukamilika jambo ambalo limeleta sintofahamu kubwa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya klabu hiyo kuandikiwa barua wakizuiwa kuwa naye kutokana kwa kuwa imekamilisha uhamisho wa wachezaji 12 wa kigeni.

Katika ujio wa Kisinda, Yanga iliamua kumwondoa Lazarous Kambole ambaye tangu amefika ameshindwa kucheza hata mchezo wa kirafiki kutokana na majeruhi lakini TFF wamesisitiza kuwa tayari Yanga walishakamlisha mchakato wa kumuombea usajili Kambole.

Taarifa rasmi ambayo imetolewa leo na TFF imeeleza kuwa kanuni inaeleza kuwa klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozid 12.

“Usajili wa wachezaji wakigeni , hasa kwa klabu ambazo timu zao zinacheza mashindano ya kimataifa ulishapitishwa na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF).

“Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji katika mazingira maalumu ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji wa kigeni ili wawahi usajili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, (CAF).

“Wachezaji wote wa klabu hizo Azam FC, Geita Gold, Simba na Yanga walishapewa leseni zao kwa ajili ya msimu wa 2022/23 ambazo ndizo imetumika kuwaombea usajili kwa ajili ya mashindano ya CAF,” ilieleza taarifa hiyo