MSHAMBULIAJI namba moja wa Yanga, Fiston Mayele ameweka wazi kuwa msimu wa 2022/23 utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kujipanga kufanya vizuri.
Nyota huyo msimu wa 2021/22 alitupia mabao 16 na pasi nne kwenye ligi huku namba moja akiwa ni George Mpole ambaye alitupia mabao 17 na pasi nne.
Nyota huyo ameweka wazi kwamba anatambua msimu mpya utakuwa ni wenye ushindani nao watapambana kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
“Kila mmoja anatimiza majukumu yake na ninatambua kuwa utakuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa ndani ya ligi.
“Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo kwenye mechi zetu hilo lipo wazi na wachezaji tunashirikiana kupata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza,” amesema Mayele.
Mshambuliaji huyo ametupia mabao mawili msimu huu kwenye ligi aliwafunga Coastal Union na Polisi Tanzania bao mojamoja.
Kwa sasa timu hiyo inajiandaa kuikabili Azam FC kwenye mchezo wa ligi ujao unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6,2022 Uwanja wa Mkapa.