TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kuwania kufuzu CHAN.
Dakika 45 za mwanzo timu zote zilikwenda vyumba vya kubadilishia nguvo wakiwa hawajafungana baada ya kutoshana nguvu.
Zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kukamilika, Uganda waliweza kupachika bao kupitia kwa Travis Mutyaba dakika ya 87 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni makosa ya mabeki aliyatumia nyota huyo kuwaadhibu wachezaji wa Stars wakiwa nyumbani.
Kim Poulsen, Kocha Mkuu wa Stars amesema kuwa makosa ambayo wameyafanya yamesababisha wapoteze mchezo wa leo.
Stars ina kibarua cha kusaka ushindi ugenini kwenye mchezo wa pili amao utaamua nani atakata tiketi ya kufuzu CHAN mashindano yanayohusu wachezaji wa ndani.