KIUNGO WA KAZI NGUMU SIMBA KUKOSEKANA MECHI MBILI

SADIO Kanoute, kiungo wa kazi ngumu ndani ya Simba hayupo na timu nchini Sudan kutokana na kupewa ruhusa maalumu kuelekea nchini Mali kushughulikia pasi yake ya kusafiria.

Simba imeweka kambi kwa muda nchini Sudan ambapo wamealikwa kwenye mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Klabu ya Al Hilal.

Anatarajiwa kukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko na ule dhidi ya Al Hilal baada ya kupewa ruhusa na uongozi.

Ikumbukwe kwamba kikosi cha Simba kilikwea pipa Alhamisi na kuibukia nchini Sudan kikiwa na msafara wa wachezaji 19 ikiwa ni pamoja na Clatous Chama, Sadio Kanoute, Peter Banda na Vicctor Ackpan.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kiungo huyo hayupo kwenye kikosi ambacho kimekwenda Sudan.

“Ni kweli kiungo wetu Sadio Kanoute hayupo kwenye sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kimesafiri kuelekea Sudan kwa ajili mashindano ambayo yameandaliwa na Al Hilal kutokana na kupewa ruhusa ili ashughulikie pasi yake ya kusafiria,”.