Arsenal Watupwa Nje FA Baada ya Kichapo Kutoka kwa Southampton

Klabu ya Arsenal imeondoshwa kwenye michuano ya FA Cup baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Southampton katika mchezo wa robo fainali.

Matokeo hayo yanaifanya Southampton kufuzu hatua ya nusu fainali, ikiungana na Manchester City na Chelsea.

Kwa upande wa Arsenal, hii ni pigo lingine kubwa baada ya kupoteza mechi ya pili mfululizo kwenye michuano ya vikombe, kufuatia kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Manchester City kwenye fainali ya Carabao Cup takribani wiki mbili zilizopita.

Katika mchezo huo:

  • ⚽ Dakika ya 35: Stewart aliifungia Southampton bao la kwanza
  • ⚽ Dakika ya 68: Viktor Gyökeres aliisawazishia Arsenal
  • ⚽ Dakika ya 85: Charles alifunga bao la ushindi kwa Southampton

Matokeo haya yanazidi kuongeza presha kwa Arsenal huku ndoto zao za kutwaa kombe msimu huu zikizidi kufifia.