Prince Dube amerejea kazini

PRINCE Dube mshambuliaji wa Yanga SC amerejea kazini mara baada ya kukosekana kwa muda kutokana na kutokuwa fiti.

Dube ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Pedro Goncalves alikosekana kwenye mchezo wa ligi vs Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Katika mchezo huo mabingwa watetezi waligawana pointi mojamoja na Mtibwa Sugar ubao uliposoma Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC.

Goli la Yanga SC lilifungwa na Pacome na lile la Mtibwa Sugar lilifungwa na Ismail Aidan kwa pigo la kona lililozama mazima ndani ya nyavu.

Dube ndani ya ligi amefunga magoli 6 sawa na Depu ambaye naye ameanza mazoezi hivyo wachezaji hawa wanatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons, Aprili 4, 2026, Uwanja wa KMC Complex.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.