Simba SC vs Coastal Union kesho inapigwa

Simba SC vs Coastal Union kesho inapigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo saa 1:00 usiku kwa wababe hawa kupambania pointi tatu.

Tayari wapinzani wa mnyama, Coastal Union wapo katika ardhi ya Dar kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo.

Hussen Mchovu, maarufu kama Diego, Ofisa Habari wa Coastal Union amesema kuwa wamefika na orodha ya wachezaji 24 tayari kuwakabili wapinzani wao kwenye mchezo wa NBC Premier League.

Kwenye msimamo Coastal Union ipo nafasi ya 13 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 15 kibindoni. Inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili na pointi 31.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.