Tanzania vs Liechtenstein ni leo kwenye FIFA Series ambayo mashindano maalum, yaliyo kwenye kalenda ya FIFA.
Mashaindano haya yanalenga kuhakikisha timu zinajiandaa na mashindano mbalimbali makubwa yanafanyika nchini Rwanda.
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Tanzania amesema wapo tayari kwa mchezo wa leo kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kukabiliana na Liechtenstein.
Tanzania imesafiri na kikosi cha mastaa 23 kwa ajili ya mashindano hayo huku wiga Simon Msuva akikosekana kutokana na sababu za changamoto za usafiri.
Gamondi amesema: “Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu, wachezaji wanatambua umuhimu wa kupata ushindi hivyo nina amini watapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,”.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.