Singida Black Stars vs Azam FC kwenye NBC Premier League inatarajiwa kupigwa Aprili Mosi, 2026 kwa wawili hawa kusaka pointi 3 muhimu ndani ya dakika 90.
Ni Uwanja wa Airtel mchezo huu utachezwa ampao wenyeji ni Singida Black Stars watawakaribisha Azam FC kwenye mchezo wa ligi.
Wenyeji Singida Black Stars kwenye mechi mbili zlizopita Machi wakiwa nyumbani walipoteza zote. Matokeo ilikuwa ni Singida Black Stars 0-3 Yanga SC na Singida Black Stars 1-2 Simba SC.
Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars amesema kuwa wanatambua ugumu wa mchezo huo na watapambana kupata pointi tatu muhimu.
“Tumekuwa na matokeo ambayo sio mazuri kwenye mechi zetu zilizopita, tulipoteza dhidi ya Yanga SC na Simba SC. Mchezo wetu dhidi ya Azam FC tutapambana kuvuna pointi tatu nyumbani,”.
Singida Black Stars kwenye msimamo ni nafasi ya 6 ikiwa na pointi 25 inawakaribisha Azam FC walio nafasi ya tatu na pointi 29.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.