Yanga SC yadunda na rekodi yake, Pedro kujadiliwa

Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Pedro Goncalves inaendelea kundunda na rekodi yake kuwa miongoni mwa timu ambazo hazijafungwa ndani ya NBC Premier League, 2025/26.

Timu hiyo imecheza jumla ya mechi 16 ikipata ushindi kwenye mechi 11, sare 5 ikiwa haijapoteza mchezo.

Imekusanya jumla ya pointi 38 ndani ya ligi mchezo wake wa 16 iligawana pointi mojamoja na Mtibwa Sugar kwa kufungana goli 1-1.

Leo uongozi wa timu hiyo unakutana na kufanya tathmini ya mechi ambazo zimepita ili kujua wapi walikwama na wapi walifanikiwa.

Taarifa zimekuwa zikieleza kuwa kuna uwezekano wa kujadili mwendo wa kocha huyo katika mechi za ligi kutokana na kushindwa kuongoza kikosi hicho kupata matokeo mazuri.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.