Sunderland Waibuka na Ushindi wa 2-1 Dhidi ya Newcastle kwenye Dabi ya Tyne-Wear

Sunderland AFC wameonyesha ubabe wao baada ya kutoka nyuma kwa bao 1-0 na hatimaye kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Dabi ya Tyne-Wear uliopigwa kwenye dimba la St. James’ Park.

Newcastle ndio walioanza kupata bao mapema dakika ya 10 kupitia kwa Anthony Gordon, lakini Sunderland walirejea mchezoni kwa nidhamu na mbinu bora.

Dakika ya 57, Talbi alisawazisha kwa Sunderland, kabla ya Brian Brobbey kufunga bao la ushindi dakika ya 90 na kuwapa wageni pointi zote tatu muhimu.

Ushindi huo unaifanya Sunderland kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya Newcastle, wakiwa hawajapoteza katika Dabi hiyo kwa mechi 11 mfululizo katika Ligi rekodi ambayo ni ndefu zaidi kihistoria katika ushindani huo mashuhuri nchini England.

Matokeo hayo yanaongeza presha kwa Newcastle, huku Sunderland wakiendelea kuonyesha ubora wao katika msimu huu wa ligi.