Mtibwa Sugar kamili kuikabili Yanga SC

Awadhi Juma, kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar amesema wamefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Yanga SC.

Mtibwa Sugar kwenye msimamo ipo nafasi ya 9 pointi 21 baada ya mechi 16 inawakaribisha vinara Yanga SC wenye pointi 37 baada ya mechi 15.

Awadhi amesema: “Tunatambua ni mchezo mgumu kulingana na ratiba hasa ukizingatia kwamba kuna mechi ambazo tulicheza Uwanja wa Jamhuri hatukupata matokeo. Tunawaheshimu wapinzani na tutaingia kwa tahadhari kwenye mchezo wetu.

“Maandalizi yamekwenda vizuri kwa asilimia kubwa hilo lipo wazi kwa kuwa tulipata muda wakufanyia kazi makosa ambayo yalipita. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kutushangilia katika mchezo wetu,”.

Mtibwa Sugar yenye nyota kama Ismail Mhesa, Magata, Mkopi na Chicharo baada ya mechi 16 imepoteza jumla ya mechi 5, ushindi kwenye mechi 5 na sare 6 inakutana na Yanga SC ambayo haijapoteza mchezo kati ya mechi 15 ikishinda 11 na sare 4.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.