Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC NBC Premier League, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma matokeo ya dakika 90 za mchezo.
Katika mchezo wa leo Machi 21,2026 wenyeji wamesawazisha kipindi cha pili baada ya kuruhusu goli mapema kipindi cha kwanza ndani ya dakika 25.
Yanga SC walianza kufunga goli la ufunguzi dakika ya 23 ya mchezo kupitia kwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua lililodumu mpaka dakika ya 89.
Mtibwa Sugar wamesawazisha goli dakika ya 90+2 kupitia kwa kiungo Ismael Mhesa kwenye muda wa nyongeza.
Kiungo huyo alianzia benchi kwenye mchezo wa leo uliokuwa na ushindani mkubwa huku vinara Yanga SC wakikwama kuvuna pointi tatu katika mchezo wa tatu mfululizo.
Matokeo haya yanaifanya Yanga SC kufikisha jumla ya pointi 38 baada ya mechi 16 wanaongoza ligi huku Mtibwa Sugar nafasi ya 7 pointi 22 baada ya mechi 17.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.