TRA United Wanasubiri Simba SC Katika Mchezo wa Kusisimua Leo

Ligi Kuu ya Soka ya NBC Tanzania bara inaendelea leo, Machi 14, 2026, kwa mechi moja ya kusisimua ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, watakuwa ugenini kukabiliana na Wakusanya Kodi, TRA United. Mchezo huu utachezwa katika Sheikh Amri Abeid Memorial Stadium, Kaloleni, Jijini Arusha kuanzia saa 4:00 jioni.

Simba SC wanakuja kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida Black Stars, ushindi wao wa kwanza baada ya sare mbili mfulululizo. TRA United nao wanajivunia ushindi wa mechi mbili mfulululizo – 4-1 dhidi ya Fountain Gate FC na 2-0 dhidi ya Namungo FC.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua, kwani timu zote zina hamu ya kuongeza pointi na kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi. Mashabiki wanatarajiwa kuhudhuria kwa wingi, huku msisimko ukiwa mkubwa kutokana na rekodi nzuri za pande zote mbili katika mechi zao za hivi karibuni.