Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kwamba Kombe la Dunia la FIFA 2026, litakaloandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada, na Mexico, litakuwa tukio bora kabisa na salama kabisa la michezo katika historia ya Marekani.
Trump alisisitiza kwamba Serikali yake inafanya maandalizi makubwa kuhakikisha usalama na mafanikio ya mashindano haya makubwa zaidi ya soka duniani. Ili kufanikisha hili, alielekeza kuanzishwa kwa Kikosi Maalum cha Ikulu kitakachoratibu juhudi za maandalizi, kikiwa na jukumu la kushirikiana na wizara na mashirika mbalimbali ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha mashindano hayo yakuwa salama, yenye utaratibu, na yanayokubalika kwa pande zote.
Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kuwa tukio kubwa sana lenye timu 48 zilizofuzu, mechi 104, na litafanyika katika miji 16 za wenyeji, likivutia mamilioni ya mashabiki wa soka kutoka duniani kote.