Rekodi zinaonyesha kuwa namba moja kwa hati safi ndani ya NBC Premier League ni Djigui Diarra wa Yanga SC akiwa nazo 7.
Erick Johora wa Mashujaa yeye ni namba mbili kwa makipa wenye hati safi zakutosha akiwa ana hati safi 6.
Ally Salim wa Dodoma Jiji, Yona Amosi wa Pamba Jiji FC na Mussa Mbisa wa Tanzania Prisons kila mmoja ana hati safi 5.
Ni timu mbili pekee ambazo hazijapoteza mechi ndani ya msimu wa 2025/26 ambazo ni Yanga SC mabingwa watetezi wa ligi na Azam FC matajiri wa Dar.
Wababe hawa wawili wanatarajiwa kukutana Machi 15 itakuwa Azam FC vs Yanga SC, Uwanja wa Azam Complex.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.