Singida Black Stars vs Yanga SC ni leo

Singida Black Stars vs Yanga SC ni leo NBC Premier League, Uwanja wa Airtel kwa wababe hawa kusaka pointi tatu muhimu.

Yanga SC 0-0 Simba SC ni matokeo yaliyopita kwa wapinzani wa Singinda Black Stars iliyo nafasi ya 9 na pointi 19.

Wageni wamekusanya pointi 29 wote wakiwa wamecheza mechi 11 ndani ya msimu wa 2025/26 wenye ushindani mkubwa.

Singida Black Stars imetoka kupata ushindi wa goli 1-0 vs Coastal Union kwenye mchezo wa ligi uliopita.

Goli la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Guede mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC.

Rekodi zinaonyesha kuwa makipa wa timu walitwaa tuzo ya man of the match, kwa Yanga SC alikuwa Djigui Diarra na kwa S.B.S alikuwa ni Metacha Mnata.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.