MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano Ali Kamwe amefichua kuwa mchezaji wa Simba SC, Seleman Mwalimu alipaswa kufungiwa mechi 5 kutokana na tukio la kuonekana akimpiga kiwiko mchezaji wa Dodoma Jiji FC.
Machi Mosi 2026, Mwalimu alianzia benchi kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi alipoingia alipata nafasi yakufunga goli ambalo lilifutwa kwa tafsiri ya mwamuzi kudai kuwa alikuwa ameotea.
Kamwe amesema: “Tukio la goli la Selemani Mwalimu, kwanza ilikuwa ‘OFFSIDE’ pili akaushika mpira. Mchezo ukaruhusiwa kuendelea kama hakijatokea kitu. Sitaki kabisa kukumbusha kuwa mchezaji huyu alitakiwa kufungiwa mechi 5, kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Dodoma Jiji.
“Sitaki kuwakumbusha, kuwa Waamuzi walishatishiwa kufungiwa maisha kimpira na kupelekwa jela kuhusu mechi hii,”.
Yanga SC ni vinara kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 29 huku Simba SC nafasi ya 3 na pointi 24 wote wamecheza mechi 11 msimu wa 2025/26.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.