Meridianbet Yaungana na TAB Kuwainua Watu Wenye Ulemavu

 

Katika kuadhimisha dhamira yake ya kujenga jamii jumuishi, Meridianbet Tanzania imefanya ziara maalum katika ofisi za Tanzania Association of the Blind (T.A.B) zilizopo Kinondoni, Dar es Salaam, na kukabidhi msaada wa fimbo za kutembelea kwa watu wenye ulemavu wa kuona. Tukio hilo limeacha alama ya matumaini na mshikamano, likionesha kwa vitendo namna sekta binafsi inavyoweza kuwa chachu ya mabadiliko ya kijamii.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa T.A.B, wanachama wa chama hicho pamoja na timu ya Meridianbet iliyoongozwa na Afisa Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Nancy Ingram. Katika hotuba yake, mwakilishi wa Meridianbet alieleza kuwa kampuni hiyo inaamini kuwa mafanikio ya kweli si tu katika biashara, bali pia katika kugusa na kubadilisha maisha ya watu kwa njia chanya.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Tofauti na misaada ya kawaida, mpango huu umejikita katika kuwezesha uhuru wa mtu binafsi. Fimbo za kutembelea zitawasaidia wanufaika kuimarisha uwezo wao wa kujitegemea, kuongeza usalama wanapotembea na kupanua wigo wa ushiriki wao katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Hii ni hatua inayolenga si tu kutoa msaada, bali kuweka mazingira ya fursa sawa kwa wote.

Mwenyekiti wa T.A.B aliishukuru Meridianbet kwa kutambua umuhimu wa kuwainua watu wenye ulemavu wa kuona, akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya taasisi na makampuni binafsi ni daraja muhimu la kufikia maendeleo endelevu. Aliongeza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka na utaleta athari chanya kwa wanachama wao.

Kupitia mpango huu wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Meridianbet inaendelea kudhihirisha misingi yake ya kurudisha kwa jamii na kujenga mahusiano imara na wadau mbalimbali. Kampuni imeeleza nia yake ya kuendeleza juhudi kama hizi, ikiamini kuwa jamii yenye usawa na kujali ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli.