Azam FC warejea Bongo na ushindi

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC wamerejea Tanzania wakiwa na zawadi ya ushindi wakiwa ugenini.

Januari 25,2026 ubao ulisoma Nairobi United 1-2 Azam FC magoli yakifungwa na Jephte Kitambala dakika ya 17 na Ernest Mohamed alijifunga dakika ya 78. Goli pekee la Nairobi United lilifungwa dakika ya 14 na Dancan Oluoch Uwanja wa Nyayo, Kenya.

Mapema Januari 26, msafara wa Azam FC umerejea Dar kwa maandalizi ya mechi zijazo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na CAF.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge amesema kuwa walikuwa wanahitaji alama tatu jambo ambalo wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Tulikuwa tunahitaji alama tatu kwenye mchezo wetu na imekuwa hivyo pongezi kwa wachezaji namna ambavyo wamejituma bila kuchoka,”.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa malengo makubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ni kupata matokeo mazuri jambo ambalo linafanyiwa kazi na benchi la ufundi.

“Kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri, hilo linawezekana kutokana na benchi imara na wachezaji kujituma bila kuchoka,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.