Al Ahly vs Yanga SC CAF Champions League ni Januari 23,2026 ambapo wababe hawa wawili wanatarajiwa kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu hatua ya makundi.
Msafara wa Yanga SC umeshatia timu Misri kwa maandalizi ya mwisho chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves akiwa na wachezaji wapya miongoni mwao ni Depu na Allan Okelo.
Goncalves ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya wapinzani ambao wanakutana nao uwanjani.
“Kila mechi tunaingia kwa lengo la kushinda. Huo ndio mtazamo wetu. Tuko kwenye mchakato wa maendeleo, na tangu nilipojiunga na timu, tumepiga hatua kubwa. Matokeo yanaonyesha hilo, lakini muhimu zaidi ni maendeleo ya jumla ya timu.
“Kuhusu wachezaji, tunataka kila mmoja ajisikie kama yuko nyumbani. Tuna malengo ya pamoja na ndoto za kufanikisha mambo makubwa kama timu. Tunatanguliza malengo ya klabu kuliko mambo binafsi”.