RASMI Januari 19, 2026 Simba SC imemtambulisha mchezaji mpya katika dirisha dogo ambaye ni beki Nickson Kibabage.
Kibabage anatambulishwa na Simba SC akitokea Klabu ya Singida Black Stars alipokuwa mwanzo wa msimu wa 2025/26.
Taarifa rasmi iliyotolewa mapema na Singida Black Stars ilibainisha kuwa wamefikia makubaliano na Simba SC ambapo wanamtoa mchezaji huyo bila malipo ili awe kwenye majukumu mapya ndani ya kikosi cha Simba SC.
Chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker Kibabage anakwenda kuongeza nguvu kwenye timu hiyo ambayo haijawa kwenye mwendo bora ndani ya msimu wa 2025/26.
Mchezaji mwingine ambaye ametambulishwa Simba SC dirisha dogo ni Libasse Gueye alitambulishwa Januari 17,2026.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.