Hiki hapa kikosi cha Simba SC vs Azam FC

SIMBA SC itakaribishwa na Azam FC kwenye mchezo wa NMB Mapinduzi Cup ikiwa ni hatua ya nusu fainali Januari 8,2026.

Chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker ni Mzizima Dabi inakwenda kupigwa Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar kwa wababe wawili kusaka ushindi.

Kikosi cha kwanza ni Hussen Abel, Duchu, Mligo, Chamou, De Reuck, Kante, Jean Ahoua, Naby Camara, Jonathan Sowah, Neo Maema na Ellie Mpanzu.

Wachezaji wa akiba ni Alexander, Mbegu, Vedastus, Semfuko, Joshua Mutale, Mzamiru Yassin, Baraka, Steven Mukwala, Awesu, Chasambi, Bajaebr.

Mshindi wa mchezo wa leo atakata tiketi kutinga hatua ya fainali ambapo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Singida Black Stars vs Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa Januari 9, 2026.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.