BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves amerejea uwanjani baada ya kuwa nje akipambania kurejea kwenye ubora.
Ni Yao Attohoula ambaye alikuwa nje kwa muda wa miezi 8 bila kucheza mchezo wa ushindani licha ya kuanza mazoezi bado hakuwa kamili kucheza mechi uwanjani.
Alirejea rasmi uwanjani Januri 6 2026 kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya TRA United ambapo kwenye mchezo huo Yanga SC ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Ecua.
Yanga SC inatarajiwa kumenyana na Singida Black Stars, Januari 9 2026 kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, kusaka mshindi atakayecheza fainali.
Huenda Yao akawa sehemu ya kikosi kwenye mchezo wa nusu fainali ambapo mchezo wake wa kwanza 2026 alichukua nafasi ya Kibwana Shomari.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.