Akina Mama Sinza Watabasamu Kupitia Msaada wa Meridianbet Hospitali ya Palestina

 

Meridianbet imeendelea kuonesha uso wake wa kibinadamu kwa kugusa moja kwa moja maisha ya mama na mtoto, baada ya kutoa msaada wa Mama Packs katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza, Dar es Salaam. Msaada huo ulitolewa kwa akina mama wajawazito na waliojifungua hivi karibuni, ukiwa na lengo la kuwasaidia katika kipindi nyeti cha uzazi na mwanzo wa malezi ya watoto wao.

Mama Packs zilizotolewa zilijumuisha mahitaji muhimu ya kila siku kama nguo za watoto wachanga, nepi, wipes, sabuni pamoja na taulo za kike, vitu ambavyo ni vya msingi lakini mara nyingi huwa changamoto kwa familia nyingi. Kupitia msaada huo, Meridianbet imechangia kupunguza mzigo wa gharama kwa akina mama wanaohudumiwa katika hospitali hiyo.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Afisa Mawasiliano wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisema kuwa kampuni imekuwa ikitambua umuhimu wa kuwekeza katika afya ya jamii, hususan kwa mama na mtoto. Alieleza kuwa msaada huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mwaka kwa vitendo vyenye manufaa kwa jamii, akisisitiza kuwa lengo ni kuleta faraja, matumaini na tabasamu kwa akina mama husika.

Kwa upande wao, viongozi wa Hospitali ya Palestina walieleza kuwa msaada huo umeongeza motisha kwa wahudumu wa afya na faraja kwa wagonjwa. Mwakilishi wa hospitali hiyo alisema hatua ya Meridianbet ni mfano wa ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na taasisi za afya, ushirikiano unaochangia kuboresha huduma na mazingira ya wagonjwa.

Hatua hiyo imeendelea kuimarisha taswira ya Meridianbet kama kampuni inayotambua wajibu wake kwa jamii. Mbali na shughuli zake za kibiashara, Meridianbet imekuwa ikijihusisha na miradi mbalimbali ya kijamii inayolenga afya, elimu na michezo, ikionesha kuwa maendeleo ya biashara yanaweza kwenda sambamba na mchango chanya kwa jamii inayozunguka