Kocha mpya Simba SC tayari kwa kazi

Kocha Mkuu wa Simba SC Steve Barker amewasili nchini kwa maandalizi ya mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Desemba 29,2025 Barker aliwasili Tanzania akiwa na wasaidizi wawili wapya tayari kwa kuwafundisha wachezaji wa timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi.

Simba SC imetoka kuachana na Meneja Mkuu, Dimitar Pantev na benchi lake la ufundi kutokana na mwendo wa timu hiyo kuwa wenye kusuasua.

Baada ya kusitisha mkataba mikoba ilikuwa mikononi mwa Seleman Matola kocha mzawa ambaye aliwahi kucheza kikosi cha Simba SC.

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Zubeda Sakuru alipata muda wa kuzungumza na kocha huyo ambaye ataanza kazi rasmi 2026.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.