INAELEZWA kuwa Yanga SC wamefikia hatua nzuri kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, ambaye bado kijana.
Kijana huyo mwenye maiaka 25 alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC msimu uliopita ilikuwa ngumu kumpata kutokana na kanadarasi yake kuwa ya mwaka mmoja.
Kwa sasa ni miezi sita inatajwa kusalia huku Yanga SC wakiwa wanapewa asilimia kubwa kuipata saini yake kwenye dirisha dogo la usajili.
Uongozi wa Yanga SC unafanya mazungumzo ya moja kwa moja na kiungo mshambuliaji wa Vipers ili kuona namna gani atajiunga na timu hiyo.
Kilichobaki ni upande wa makubaliano kwa pande zote mbili na kusaini mkataba mpya ikiwa makubaliano yatafika kwenye hatua nzuri.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.