Man United yawachapa Newcastle, yapanda hadi nafasi ya tano

Mashetani Wekundu wa Manchester United wameibuka na ushindi wa 1–0 dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa Old Trafford, na kujihakikishia alama tatu muhimu.

Goli pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 24 na Dorgu, likitosha kuwapa United pointi zote.

Kwa matokeo hayo, Manchester United imefikisha alama 29 baada ya mechi 18, na kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

FT: Man United 1–0 Newcastle United
⚽ 24’ Dorgu