AFCON 2025: Uganda 1-1 Tanzania, Msuva atwaa tuzo

MCHEZO wa pili kati ya mitatu katika hatua ya makundi umekamilika kwa wababe wawili kutoshana nguvu na kugawana pointi mojamoja.

Baada ya dakika 90 nchini Morocco leo Desemba 27 2025 ubao umesomaUganda 1-1 Tanzania wakigawana pointi katika kundi C.

Tanzania ilianza kupata goli la kuongoza dakika ya 59 kupitia kwa nyota Simon Msuva ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati.

Goli hilo lilidumu mpaka dakika ya 80 baada ya Uganda kupata goli la kuweka mzani sawa kupitia kwa U. Ikpeazu.

Tanzania inavuna pointi moja kwa mara ya kwanza baada ya mchezo wa kwanza kupoteza dhidi ya Nigeria na Uganda pia wanapata pointi kwa mara ya kwanza baada ya mchezo wa kwanza kupoteza dhidi ya Tunisia wenye pointi tatu.

Mchezaji wa Tanzania Simon Msuva amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.