Prince Dube na rekodi yake AFCON 2025

PRINCE Dube mshambuliaji namba moja wa kikosi cha Yanga SC ameandika rekodi yake kwa msimu wa 2025/26 kwenye mashindano makubwa Afrika.

Dube yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya Zimbabwe alianza kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya Misri ambao ni wa hatua ya makundi.

Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Misri 2-1 Zimbabwe ambapo rekodi ya Dube ni kufunga bao la kwanza kwa wachezaji wanacheza Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Licha ya kufunga bado haikuwa rahisi kwa Zimbabwe kukomba pointi tatu kwenye mchezo huo muhimu kwa kuwa wababe Misri waliibuka na ushindi.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.